ZIJUE FAIDA KUU 4 ZA MAFUTA NA MAJANI YA MVUJE KATIKA MWILI WA BINADAMU
mvuje
Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akishika Mmea wa Mvuje na kupata maelezo yake
Mpenzi msomaji siku ya leo nimekuletea ujumbe mzuri kutoka kwa Dokta Bingwa wa tiba asili Afrika Mashariki na kati, Suleiman Bin mzee, kuhusiana na faida kuu 4 za mafuta ya mvuje.
Anaeleza kwamba majani haya haswa yalianza kuoteshwa bara hindi na baadae yalipojulikana matumizi na matumizi na faida zake zilichukuliwa mbegu zake na kusambazwa ulimwenguni. Uzuri wa mbegu za majani ya mvuje zinaota popote pale.
FAIDA ZA MAFUTA YA MVUJE YATOKANAYO NA MAJANI YAKE
Huondoa degedege kwa watoto
Mafuta yake ni kinga dhidi ya Jinamizi
Wale wenye tatizo la kuota ndoto mbaya mpatie mafuta ya Mvuje
Maradhi ya kupooza viungo vya mwili(kupararaizi).
FAIDA NA MATUMIZI YA MAJANI YA MVUJE
KUONDOA MADOA NA CHUNUSI : Unatwanga majani yake kisha unakamulia maji ya ndimu na kuyapaka usoni inaondoa machunusi na madoa sugu usoni. Unapakaa kila siku mara 1 mpaka madoa yanapotea.
Unatwanga majani yake na kuychanganya na binzari manjano na Unapakaa usoni kwajili ya kuua chunusi usoni na kuondoa na kuziba chunusi nyingine ambazo zinakua zinataka kujotokeza.
Mchanganyiko huu haswa umewasaidia watu wengi kuua chunusi usoni na mabegani na mgongoni. Pakaa kila siku mara moja mpaka chunusi zinapotea.
KUPUNGUZA UZITO : Pia unaweza kuchukua fungu moja la majani ya mvuje na kusaga na maji katika blender na kumimina kwenye glass na unakorogea kijiko 1 cha asali kwajili ya kupunguza uzito na pia kuondoa cholesterol.
MBOGA : Ukitaka kupata unga wake unakausha majani juani mpaka yanakua makavu, kisha unayatwanga na kuyachunga na kuweka katika kopo safi na kavu. Inafaa kutumia katika michuzi na roast
By tibazetutz@gmail.com